AJALI YA LORI LA MATOFALI LAUWA WATATU,

WATU watatu wamefariki dunia kwa ajali iliyotokea mapema hii leo mkoani Mwanza maeneo ya Mataa Nyakato - sokoni. Tukio lililohusisha lori lililokuwa limebeba matofali kufeli breki wakati wa kushuka kuelekea Nyakato National na hivyo kwenda kuyagonga magari yaliyokuwa yakisubiri ruhusa ya taa za kuongozea magari.

Magari matatu ya abiria (Hiace) na gari moja private yamehusika katika ajali hiyo. Dalali maarufu hapa Mwanza anaefahamika kwa jina la Mzee Shaaban Kumba ndiye mwenye gari private iliyogongwa ambaye amefariki papo hapo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa anashuka na taarifa zaidi kwa kina.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii