Watu 57 waliokuwa mateka wa ADF waunganishwa na familia zao DRC

Watu 57 waliokuwa wanashikiliwa mateka na kundi la waasi la Allied Democratic Forces-ADF mashariki mwa Kongo wamekutanishwa na familia zao jana Jumamosi. Miongoni mwao wanawake waliokuwa wakitumiwa kama watumwa wa vitendo vya ngono, waliachiliwa huru mwishoni mwa juma baada ya operesheni kubwa ya kijeshi baina ya wanajeshi wa Kongo na Uganda, kuwapa nafasi ya kutoroka mikononi mwa ADF. Sherehe ya kuwaunganisha tena mateka hao wa zamani na familia zao ilifanyika mjini Beni, huko Kivu ya Kaskazin

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii