Burkina Faso yamtaka balozi wa Ufaransa aondoke

Burkina Faso imemtaka balozi wa Ufaransa kuondoka nchini humo, wakati kukiwa na ongezeko la hasira dhidi ya mkoloni huyo wa zamani wa Burkina Faso. Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa amethibitishia shirika la habari la Reuters kuwa watawala wa mpito wa Burkina Faso wamefanya ombi hilo.

Msemaji huyo amesema wizara hiyo haina kauli yoyote kuhusu ombi hilo, ambalo alielezea kuwa "utaratibu wa kawaida.

" Shirika la habari la Ufaransa AFP wakati huo huo limeripoti kuwa balozi Luc Hallade angali kazini katika mji mkuu wa Burkinabe Ouagadougou. Waburkina Faso wanailaumu Ufaransa kwa kushindwa kuzuia uasi wa itikadi kali ambao umeenea katika nchi jirani Mali na kuingia katika nchi hiyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita kabla ya mwaka mpya, makundi ya wapiganaji yanayoliunga mkono jeshi yaliwauwa watu 28 kutoka kabila la Fulani, wakiwemo watoto.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii