Japan, Marekani kuzungumzia usalama kabla ya mkutano wa Kishinda na Biden

Japan na Marekani zitafanya mkutano kuhusu usalama kati ya mawaziri wa kigeni na ulinzi mjini Washington, siku moja kabla ya Waziri Mkuu Fumio Kishida kuwasili katika mji mkuu wa Marekani wiki ijayo.

Ziara ya Marekani itakamilisha ziara ya Kishida katika kundi la nchi saba zilizoendelea zaidi kiviwanda, G7, huku Japan ikijitanua kijeshi na kuimarisha uhusiano wake na Marekani, wakati ambapo ushawishi wa China unaongezeka. Kishinda ataanza ziara yake Jumatatu ijayo nchini Ufaransa, Italia, Uingereza na Canada kabla ya mkutano wa kilele na Rais Joe Biden, Januari 13.

Waziri wa ulinzi wa Japan Yasukazu Hamada na Waziri wa Mambo ya Nje Yoshimasa Hayashi watakwenda Washington kukutana na wenzao wa Marekani Lloyd Austin na Antony Blinken kwa mazungumzo ya usalama Jumatano ijayo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii