Rwanda "Hatuwezi kuchukua wakimbizi zaidi kutoka DRC"

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amesema nchi hiyo haiwezi tena kutoa hifadhi kwa watu wanaokimbia ghasia katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

 Akizungumza jana na bunge la Rwanda mjini Kigali, Kagame amesema hilo sio tatizo la Rwanda na hawapaswi kuubeba mzigo huo.

 Mara kwa mara Rwanda imeishutumu Kongo kwa mzozo huo na imeishutumu jumuiya ya kimataifa kwa kufumbia jicho hatua ya Kongo kuliunga mkono kundi la waasi kutoka Rwanda la FDLR.

Rwanda pia imeishutumu Kongo kwa kuutumia mzozo huo kwa madhumuni ya kisiasa pamoja na kile ilichosema ilitunga kuhusu mauaji ya mwezi Novemba ya raia wapatao 131. 

Umoja wa Mataifa umewashutumu waasi wa M23 kwa kuhusika na vifo hivyo. Kongo pamoja na Marekani na nchi kadhaa za Ulaya zimekuwa zikiishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono M23, ingawa Rwanda inakanusha madai hayo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii