Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, amependekeza kubuniwa kwa mahakama maalum ya kimataifa ili kuwashitaki viongozi wa Urusi.Baerbock aliutaja ‘uvamizi wa Urusi nchini Ukraine’ kama ukiukwaji wa sheria ya kimataifa.
Alitoa pendekezo hilo alipozuru Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC mjini The Hague nchini Uholanzi.
Amesema pendekezo hilo lilijadiliwa na mwenzake wa Ukraine wakati alipofanya ziara ya kushtukiza mashariki mwa Ukraine wiki iliyopita.
Mahakama ya ICC imetuma wataalamu wake nchini Ukraine kuchunguza uwezekano wa uhalifu wa kivita.
Hata hivyo Urusi haijaidhinisha mkataba wa Roma unaoipa mahakama hiyo mamlaka ya kuiwajibisha. Na kwa upande mwingine Ukraine pia haijajiunga kikamilifu na mahakama ya ICC