Waziri Mkuu wa New zealand Jacinda Ardern atangaza kujiuzulu mwezi ujao

Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern, ametangaza kuwa atajiuzulu wadhifa huo ifikapo tarehe saba mwezi ujao.Kwenye taarifa yake iliyotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni, Ardern amesema hana mipango ya kuwania wadhifa huo kuchaguliwa tena katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 14.

Ameongeza kuwa anaamini chama chake cha Labour, kitashinda uchaguzi ujao, na kwamba kiongozi mpya wa chama hicho atachaguliwa siku ya Jumapili.Naibu wake Grant Robertson ambaye pia ni waziri wa Fedha amesema kupitia taarifa kuwa hatagombea kuwa kiongozi mpya wa chama hicho tawala.Ardern alichaguliwa kuwa Waziri mkuu wa New Zealand mwaka 2017 alipokuwa na umri wa miaka 37, hivyoa kuwa moja kati ya wanawake wenye umri mdogo ulimwenguni kuongoza serikali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii