Ujerumani haitoizuia Poland kupeleka vifaru vya Leopard Ukraine

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema Ujerumani haitoizuia Poland iwapo inataka kupeleka vifaru chapa Leopard 2 nchini Ukraine.

Kauli hii hii ya Baerbock huenda ikaleta matumaini kwa Ukraine ambayo inahitaji vifaru hivyo kwa ajili ya mapambano yake na Urusi.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani ameyasema haya alipokuwa akizungumza na televisheni moja nchini Ufaransa.

Matamshi yake lakini yanaonekana kukinzana na yale ya Kansela Olaf Scholz ambaye katika mkutano mmoja wa kilele mjini Paris mapema jana alisema kwamba maamuzi yote kuhusiana na kupelekwa kwa silaha Ukraine, yatatokana na makubaliano na marafiki wa Ujerumani ikiwemo Marekani.

Ujerumani imekuwa katika shinikizo kubwa kutoa idhini ya vifaru hivyo kupelekwa Ukrainen ila chama cha Scholz cha Kisoshalisti kinahofia Urusi kuzidisha mashambulizi yake baada ya hilo kufanyika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii