Utawala wa Taliban nchini Afghanistan umechukua uamuzi jana wa kuwazuia wanawake kote nchini humo kujiunga na vyuo vikuu. Serikali hiyo yenye msimamo mkali wa Kiislamu inaendelea kukiuka haki na uhuru wa wanawake ya kupata elimu. Wanawake wamepigwa pia marufuku kutembelea sehemu za mapumziko pamoja na kumbi za michezo. Uamuzi huo umeibua wasiwasi mkubwa miongoni mwa jamii ya kimataifa iliyolaani vikali ukiukwaji huo.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelaani uamuzi huo na kusema kuwa serikali ya Taliban inavunja ahadi yake ya kulegeza misimamo katika sheria zake