Wanawake wa Afghanistan waandamana kupinga kuzuiwa kusoma vyuo vikuu

Wanawake chungunzima wameandamana nje ya chuo kikuu cha Kabul nchini Afghanistan jana Alhamisi, kupinga uamuzi wa kuwazuia wanawake kujiunga na elimu ya chuo kikuu nchini humo.

Hatua ya wanawake hao ndio ya mwanzo ya maandamano makubwa ya hadhara katika mji huo, tangu Taliban ilipotangaza uamuzi wake wa kufunga vyuo vikuu kwa wanafunzi wa kike.

Hali ya usalama imeongezwa katika mji huo ndani ya kipindi cha siku kadhaa ikiwemo kwenye vyuo vikuu.

Uamuzi huo wa Taliban umekosolewa na jumuiya ya kimataifa pamoja na Saudi Arabia na Uturuki ambazo ni nchi kubwa za kiislamu.

Hata hivyo utawala wa Taliban umeutetea uamuzi wake kwa kusema waliwapiga marufuku wanawake kusoma katika vyuo vikuu kwa kiasi, kutokana na wanafunzi wa kike kutozingatia tafsiri ya kanuni ya mavazi ya Kiislamu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii