Takwimu zaonyesha ongezeko la Uviko-19

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya zimeonyesha ongezeko la wagonjwa wa Uviko-19 nchini kutoka asilimia 4.1 hadi asilimia 5.5.


Takwimu za wiki ya kwanza ya Novemba 2022 zinaonyesha watu 1,154 waliopima Uviko-19, waliokuwa wanaugua ni 47, huku takwimu za wiki ya pili zinaonyesha kati ya watu 1,294 waliopima Uviko-19, watu 71 wanaugua ugonjwa huo.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema hayo juzi, wakati akitoa tamko lake la salamu za sikukuu ya Krismasi huku akiwataka watumiaji wa vyombo vya moto kuwa makini barabarani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii