Pinda ateuliwa kwenye Baraza la kumshauri Rais

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la kumshauri Rais kuhusu utekelezaji wa masuala ya kilimo na chakula.


Taarifa ya uteuzi huo imtolewa leo Machi 14, 2023, na kwamba uzinduzi wa Baraza hilo utafanyika Machi 17 Ikulu ya Dar es Salaam.

Rais Samia pia amemteua Dkt Jacqueline Mkindi, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticulture Association (TAHA), kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Baraza la kumshauri Rais kuhusu utekelezaji wa masuala ya kilimo na chakula.

Wengine walioteuliwa kuwa wajumbe ni Dkt. Florence Turuka ambaye ni Katibu Mkuu Mstaafu na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), pamoja na Dkt Mwatima Juma, ambaye ni Mwenyekiti wa Tanzania Organic Agricultural Movement (TOAM).

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii