Mtoto wa kiume wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jeneral Muhoozi Kainerugaba, amweka wazi nia yake ya kugombea urais wa taifa hilo katika uchaguzi mkuu wa Taifa hilo mwaka 2026.
Jenerali Muhoozi, kupitia ukurasa wa mtandao wa twitter ameweka ujumbe huo huku akidhihirisha kwamba ni majibu kwa wale waliokuwwa wakihoji swala la yeye kugombea urais.
“Mmenitaka mimi kulisema daima! Sawa, kwa jina la Yesu Mungu wangu, kwa jina la vijana wote wa Uganda na dunia na kwa jina la mageuzi bora, nitagombea Urais katika mwaka 2026!” Ulisomeka ujumbe huop katiaka ukurasa wake wa Twitter.