Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza ziarani nchini Rwanda

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman yupo ziarani mjini Kigali tangu jana Jumamosi ili kutetea mpango tata wa kuwahamisha hadi Rwanda waomba hifadhi wanaowasili nchini Uingereza.


Braverman ametembelea eneo la Bwiza kunakojengwa kituo cha kuwapokea wahamiaji hao na kusema makubaliano kati ya Uingereza na Rwanda yatasaidia kutafutia suluhu ya haki na kibinaadamu katika suala la wahamiaji.


Kigali na London walifikia makubaliano ya dola milioni 146. Mwaka jana, zaidi ya wahamiaji 45,000 waliwasili kwenye pwani ya Kusini-Mashariki mwa Uingereza wakitumia mashua ndogo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 60 kila mwaka tangu mwaka 2018.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii