Wanaoshiriki ngono kwa mdomo waonywa

Jamii imetakiwa kujiepusha na mambo ambayo ni kinyume na utamaduni wa kitanzania ikiwemo kufanya ngono ya mdomo (Oral Sex) ili kuepuka vinywa vyao kupata maambukizi ya virusi hatari vya human papilloma vinavyosababisha ugonjwa wa saratani .


Dokta Emmanuel Motega ni mkuu wa idara ya kinywa na meno katika kospitali ya Rufaa ya kanda Bugando ametoa ushauri huo mara baada ya kufanya uchunguzi wa kinywa na meno kwa wakazi wa jiji la Mwanza ndipo akawaasa kuacha tabia ya kufanya ngono ya mdomo

"Wapo virus wanaitwa hypataitis na kuna wengine wanaitwa human papilloma virus hawa ni wadudu wanaopatikana sehemu za siri wakienda mdomoni wanaweza kusababisha ugonjwa unaitwa oralwhat hata kusababisha ugonjwa wa kansa kuna aina ya kansa ambazo zinatokea mdomoni ambazo zinasababishwa na hao virus ambao eneo lake linakuwa la siri ikitokea wakahama wakaja mdomoni wanaleta madhara kwa kufanya oral sex unaweza kuwahamisha wadudu waliopo sehemu nyingine wakasababisha madhara sisi kama wataalamu wa kinywa na meno hatushauri kabisa hivyo vitendo"


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii