Bunge la taifa limeshuhudia cheche za maneno baada ya wabunge wa Kenya Kwanza na wale wa Upinzani kuanza kuzozana kuhusu ni nani wa kulaumiwa katika maandamano yaliyofanyika Jumatatu 20.
Kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Kima Ichungwa alisema kuwa Raila Odinga anajifanya kupenda demokrasia ila kila mara anaenda kinyume na demokrasia yenyewe.
Matamshi ya Ichungwa yalionekana kuwakwaza wabunge wa Azimio ambao walidai kuwa matamshi hayo hayastahili na ni ya kumdhalilisha kinara wa Azimio.
Kuwa wa kwanza kupata habari motomoto kutoka kwa Mhariri wetu Mkuu JISAJILI THANK YOU! Check your email and confirm your subscription You are already subscribed to our newsletter! Check your inbox to be the first to know the hottest news Mwanzo Siasa SIASA Bunge Lachemka Wabunge wa Azimio na Kenya Kwanza Wakizozona Kuhusu Maandamano ya Jumatatu 20 Alhamisi, Machi 23, 2023 at 1:16 PM na Peter Okeah Wabunge wa mirengo miliwili hasimu ya kisiasa Azimio na Kenya Kwanza wamelaumiana kuhusu uharibufu wa mali ulioshuhudiwa wakati maandamano Kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Kimani Ichungwa amesema kuwa Raila Odinga si mwana demokrasia bali ni gaidi wa uchumi Viongozi wa upinzani wamesema kuwa maandamano yalikuwa ya amani hadi pale maafisa wa usalama walianza vurugu MAKINIKA: Tusaidie kubadilisha maisha ya wengi, jiunge na programu ya Patreon kutoka TUKO.co.ke. Bunge la taifa limeshuhudia cheche za maneno baada ya wabunge wa Kenya Kwanza na wale wa Upinzani kuanza kuzozana kuhusu ni nani wa kulaumiwa katika maandamano yaliyofanyika Jumatatu 20. Wabunge wa Azimio na Kenya Kwanza wamezozana kuhusu ni nani anayestahili kujukumika katika uharibifu unaoshuhudiwa wakati wa maandamano. Picha UGC. Chanzo: Twitter Kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Kima Ichungwa alisema kuwa Raila Odinga anajifanya kupenda demokrasia ila kila mara anaenda kinyume na demokrasia yenyewe. "Bila kumkosea heshima kiongozi wa upinzani Raila Odinga, yeye anajifanya kuwa mwana demokrasia lakini hilo si kweli kwani yeye anaweza kulinganishwa tu na gaidi wa kiuchumi," Ichungwa alisema. RECOMMENDED FOR YOU Carolyne Demathew: Ukitaka Kula Pesa Kwa Uzuri, Kula ya Babako Matamshi ya Ichungwa yalionekana kuwakwaza wabunge wa Azimio ambao walidai kuwa matamshi hayo hayastahili na ni ya kumdhalilisha kinara wa Azimio. MAKINIKA: Jinyakulie habari ZINAZOKUFAA ➡️ tafuta “IMEPENDEKEZWA KWA AJILI YAKO” na ufurahie! Cheche hizo za maneno katika bunge la taifa lilimlazimu spika wa kikao hicho Faram Maalim kumfurusha bungeni mbunge wa mrengo wa Azimio Jared Okello. Kiongozi wa Wachache katika bunge la taifa Opiyo Wandayi alisema kuwa maandamano ya Jumatatu 20 yaligeuka na kuwa na vurugu wakati ambapo polisi walianza kuwarushia waandamanaji vitoa machozi. "Maandamano ya Jumatatu yaligeuka na kuwa na vurugu kwa sababu ya vurugu waliotoa maafisa wa polisi kwa wafuasi wa Azimio," Wandayi alisema.