Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza hali ya dharura nchini humo hususan katika jimbo la Mississippi baada ya kimbunga kulikumba eneo hilo usiku wa kuamkia jumapili na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 25 huku kingine kikiripotiwa katika jimbo la Alabama.
Biden amesema familia zote zilizoathiriwa katika kaunti za Carroll, Humphreys, Monroe, na Sharkey watapatiwa fedha za kujikimu.
Dhoruba hiyo iliyodumu kwa dakika kumi imetokea usiku watu wakiwa wamelala huku kukiwa na tahadhari ya dhoruba nyingine kuzuka katika maeneo ya Alabama na Georgia.