OFISA wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF Jacqueline Kamwamu amemshataki Polisi Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez.
Mashtaka hayo yamefunguliwa katika kituo Kikuu Cha Polisi, Dar, Januari 20,2022 ambapo Barbara alipokea wito wa kufika kituoni hapo na baada ya kufika aliwekwa ndani kwa saa nane kisha kusomewa shtaka lake.
Shtaka linalomkabili Barbara ni kutoa lugha isiyopendeza kwa Afisa wa TFF Jacqueline Kamwamu ambae alimzuia asiingie Uwanjani katika eneo la VIP na Watoto wadogo siku ya December 11 2021 katika mchezo kati ya Yanga na Simba.