Rais wa Marekani, Joe Biden, amesema nchi yake itahakikisha Kenya inakuwa mwanachama wa jumuiya ya nchi za kujihami za magharibi NATO, hatua ambayo itaifanya Kenya kuwa taifa la kwanza kwenye ukanda wa jangwa la Sahara kuwa mwanachama.
Katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Marekani, rais Ruto, aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kutetea demokrasia na usalama wa ukanda na dunia.
'‘Ni sisi watu wa Kenya tuliofanya uamuzi huu kwa nia ya kutumikia amani na utulivu kama raia wa kimataifa anayewajibika.’’ Alisema rais William Ruto.
Katika ziara hiyo, mbali na kutiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano, Washington itaipa Kenya ndege za kijeshi 16 kusaidia katika operesheni zake za kulinda amani kwenye ukanda, ziara ambayo wadadisi wa mambo wanasema Nairobi itanufaika pakubwa.