Ufaransa inawaalika raia wake, haswa wale wanaopitia, nchini Lebanon kuondoka nchi hii "haraka iwezekanavyo" katika "mazingira tete ya usalama", inaandikwa kwenye tovuti ya ushauri kwa wasafiri ya Wizara ya Mambo ya nje. Paris ilikuwa tayari "ikiwahimiza" raia wake kutosafiri kwenda Lebanon.
Safari za ndege za moja kwa moja na zile za biashara kwenda Ufaransa bado zinapatikana," Quai d'Orsay imesema.
Ufaransa pia inapendekeza kwamba raia wake wanaoishi nchini Iran "waondoke nchini humo kwa muda" ikiwa wanaweza, ikibaini kuwa kuna hatari ya kufungwa kwa anga na viwanja vya ndege vya Iran. Maagizo haya yanakuja katika muktadha wa mvutano mkali na Israeli, baada ya mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyeh, aliyeuawa siku ya Jumatano Julai 31 huko Tehran, ambayo Iran ilihusisha Israel, ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas. Iran imeahidi kulipiza kisasi.
"Kwa mara nyingine tena tunatoa wito kwa raia wetu kuchukua tahadhari kubwa katika safari zao, kuepuka mikusanyiko yoyote na kujijulisha kuhusu matukio ya sasa na ujumbe au maagizo kutoka kwa Ubalozi wa Ufaransa nchini Iran katika siku zijazo", kulingana na maagizo kwa wasafiri yaliyochapishwa siku ya Jumapili.
Mauaji haya yalitokea siku moja baada ya shambulio lililomuua kiongozi wa kijeshi wa Hezbollah kutoka Lebanon, Fouad Chokr, karibu na mji wa Beirut.
Kulingana na makadirio, zaidi ya Wafaransa 23,000 wanaishi Lebanon, wakiwemo Wafaransa 21,500 na wenye haki waliosajiliwa kwenye orodha za ubalozi. Kila msimu wa joto, raia wengi wa wenye uraia pacha pia hupitia Lebanon. Mwishoni mwa mwezi wa Julai, kulikuwa na karibu Wafaransa 10,000 waliopitia Lebanon