Upinzani nchini Venezuela umeahidi kuendelea na maandamano wakati wa maandamano huko Caracas, Jumamosi Agosti 17, kwenda "hadi mwisho" kupinga kuchaguliwa tena kwa ais Nicolás Maduro mwishoni mwa mwezi wa Julai mwaka huu.
Rais Maduro kwa upande wake aliwahakikishia wafuasi wake, ambao pia walihamasishwa katika mji mkuu, kwamba hawawezi "kuwashinda" kamwe.
Hali nchini Venezuela inaendelea kutia wasiwasi, huku pande zote mbili zikionekana kupambana hadi mwisho.
Venezuela inakabiliwa na mzozo wa kisiasa uliosababishwa na ushindi wenye utata wa rais Nicolas Maduro, katika matokeo ya uchaguzi yaliyokakataliwa vikali ndani na nje ya nchi hiyo.
Kufikia sasa, maandamano ya kupinga ushindi wa Maduro yamesababisha vifo vya watu 25 huku wengine karibu 200 wakijeruhiwa na zaidi ya watu 2,400 wakikamatwa tangu ulipofanyikauchaguzi wa Julai 28.