Rais Ruto ateua mawaziri wapya 11, siku nane baada ya kufuta karibu serikali yake yote

Nchini Kenya, rais William Ruto ameteua mawaziri wapya 11 siku ya Ijumaa Julai 19, 2024 jijini Nairobi. Tangazo ambalo linajiri siku 8 baada ya William Ruto kuvunja karibu baraza lake lote la mawaziri.

"Nimeanza mchakato wa kuunda serikali mpya iliyopanuliwa ili kunisaidia kuongoza mabadiliko ya haraka na yasiyoweza kubatilishwa ya nchi yetu," amesema katika mkutano na waandishi wa habari, kabla ya kuorodhesha majina ya watu 11 waliochaguliwa, ambao wengi wao walikuwa tayari wanahudumu katika serikali iliyofutwa. 

Rais Ruto anakabiliwa na maandamano makubwa kufuatia sheria tata ya fedha na ukandamizaji mbaya wa maandamano dhidi ya muswada huo, ambao umefutiliwa mbali tangu wakati huo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii