Brazil yaomba msamaha kwa mateso ya wahamiaji wa Japan


Serikali ya Brazil iliomba msamaha kwa ukiukwaji wa haki za binadamu katika mateso na kufungwa kwa wahamiaji wa Japan katika miaka ya baada ya vita ya pili ya dunia.


Eneá de Stutz e Almeida, rais wa Tume ya Msamaha, bodi ya ushauri ya wizara ya haki za binadamu inayochambua maombi ya msamaha na fidia kwa waathiriwa wa mateso ya kisiasa nchini Brazil, ameiambia Japan kwamba anataka kuomba msahama kwa niaba ya taifa la Brazil kwa mateso, unyama wote, ukatili, chuki dhidi ya wageni na ubaguzi wa rangi uliofanywa dhidi ya raia wake.


Bodi hiyo iliidhinisha ombi hilo la kuomba msamaha katika kikao kilichofanyika mjini Brasilia na kuhudhuriwa na wanachama wa serikali ya Brazil na watu mashuhuri wa jamii ya Kijapani.


Bendera za nchi zote mbili ziliwekwa mezani wakati wa mazungumzo hayo.


Ripoti hiyo ya Tume ya Msamaha ilikiri kuwa wahamiaji 172 wa Japan, walipelekwa kwenye kambi ya mateso karibu na pwani ya São Paulo, ambako waliteswa kuanzia mwaka 1946 hadi 1948.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii