DRC: Mlipuko wa Ndui ya nyani waua zaidi ya watu 400, mamlaka yatiwa wasiwasi

Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na wataalamu wa afya wana wasiwasi kwa sababu idadi ya wagonjwa wa Ndui ya nyani, ambao pia huitwa Monkeypox, inaongezeka. Zaidi ya wagonjwa 11,000 wamerekodiwa na watu 450 wamefariki. Kati ya mikoa 26 ya DRC, 25 imeathiriwa na ugonjwa huo pia unaendelea katika nchi jirani ya Burundi, na hivyo kuongeza hofu ya kuibuka kwa aina mpya, mbaya zaidi ya virusi hivi.

Hapo awali, wagonjwa waliambukizwa na wanyama walioambukizwa, lakini aina mpya ya ugonjwa huu huambukizwa kati ya binadamu. Nchini DRC, mkoa wa Équateur (Magharibi) ndio ulioathiriwa zaidi, anabainisha msemaji wa serikali Patrick Muyaya.


"Watu wana wasiwasi kwa kweli," anaelezea Dk Cris Kasita, anayehusika na shughuli za kukabiliana na ugonjwa wa Ndui ya nyani (Monkeypox) nchini DRC. Tuna zaidi ya arifa 800 kwa wiki ya mlipuko wa Ndui ya nyani. Serikali imeamua kuweka utaratibu ili kwa pamoja tujue namna ya kukomesha janga hili ambalo linashika kasi."


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii