Algeria kuweka visa kwa raia wa Morocco kutokana na 'vitendo vinavyodhuru' utulivu wake

Algeria, ambayo haina tena uhusiano wa kidiplomasia na Morocco tangu 2021, imeamua mara moja tangu siku ya Alhamisi kuweka visa ya kuingia nchini humo kwa raia wa Morocco. Algiers inaishutumu Rabat kwa kufanya "vitendo vinavyodhuru" utulivu wake.

Algiers inaishutumu Rabat kwa kuchukua fursa ya utawala wa kutotoza viza kupeleka maafisa wa kijasusi wa Israel baada ya kupewa pasipoti za Morocco na kufanya vitendo vinavyohatarisha uthabiti na usalama wa nchi.

Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Mambo ya Nje inataja "shirika" kubwa la mitandao ya uhalifu iliyopangwa, biashara ya madawa ya kulevya na binadamu, magendo na uhamiaji haramu. Vitendo vinavyochukuliwa, kulingana na chanzo hicho, kama "tishio la moja kwa moja" kwa usalama wa nchi na "kuweka udhibiti thabiti na mkali wa maeneo yote katika ardhi ya Algeria".

"Morocco inawajibishwa pekee kwa mchakato wa sasa wa kuzorota kwa mahusiano baina ya nchi hizimbili kupitia vitendo vyake vya uhasama dhidi ya Algeria," taarifa hiyo kwa vyombo vya habari imebainisha.

Mnamo mwezi wa Agosti 2021, kama ukumbusho, Algeria ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Morocco, ikimtuhumu jirani yake kwa "vitendo vya uhasama", ikitoa mfano wa matumizi ya programu ya Israeli ya Pegasus kuwapeleleza maafisa wa Algeria.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii