Polisi nchini Pakistan wameripoti tukio la kusikitisha ambapo mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 ameuawa kwa kupigwa risasi na baba yake baada ya kugoma kufuta akaunti yake ya TikTok.
Kwa mujibu wa taarifa za uchunguzi, baba huyo alitekeleza mauaji hayo siku ya Jumanne, akidai kuwa alikuwa “analinda heshima ya familia.” Polisi walithibitisha kuwa mtuhumiwa amekamatwa na anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.
Katika tukio lingine lililotokea mwezi uliopita nchini humo, msichana mwingine mwenye umri wa miaka 17, Sana Yousaf, ambaye pia alikuwa maarufu kupitia TikTok, aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwao na mwanaume aliyemkataa kimapenzi.
Visa hivi vinazidi kuibua taharuki kuhusu usalama wa wasichana na changamoto za matumizi ya mitandao ya kijamii katika baadhi ya jamii zenye mitazamo mikali ya kitamaduni.