Mahakama yatupilia mbali maombi ya Tundu Lissu

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, aliyekuwa akitaka uamuzi wa Mahakama ya Kisutu wa kuahirisha usikilizwaji wa kesi yake ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni upitiwe upya.

Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Elizabeth Mkwizu baada ya kukubaliana na mapingamizi ya Serikali ya kwamba Mahakama Kuu haina mamlaka kwa kuwa ahirisho la mwisho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu halikumaliza kesi.

Aidha katika uamuzi wake, Mahakama Kuu imesema kuwa maombi hayo hayakuwa sahihi kufikishwa kabla ya kesi ya msingi kukamilika, hivyo yamekataliwa kwa msingi wa kisheria.

Tundu Lissu alikuwa anapinga uamuzi uliotolewa Juni 2, 2025, na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini sasa atalazimika kusubiri hadi kesi ya msingi itakapokamilika ndipo hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii