Waumini Kanisa la Gwajima ndani ya mahakama kufuatilia kesi

Waumini na viongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo la Askofu Mkuu, Josephat Gwajima, wakiwa katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo, Julai 11, 2025 ambapo Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma imewatia wadaawa katika shauri la maombi ya kikatiba, lililofunguliwa na baadhi ya waumini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church, kufika mahakamani leo.

Shauri hilo la maombi mchanganyiko limefunguliwa na Dinali Mbaga na wenzake 51 dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP).

Katika shauri hilo, waombaji hao ambao kanisa lao lipo Ubungo, Dar es Salaam wanapinga kitendo cha askari wa Jeshi la Polisi kuwazuia kukusanyika kwa ajili ya kufanya ibada na kuwatia mbaroni.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii