Chelsea yatwaa ubingwa wa dunia baada ya kuipiga PSG

Timu ya Chelsea FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Dunia baada ya kuishusha PSG kipigo cha Magoli 3-0 katika Fainali ya michuano hiyo ambayo ilishirikisha vikosi 37

Licha ya PSG ambaye ni bingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kupewa nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo, mambo yalikuwa magumu kwao. Waliofunga katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa MetLife ni Cole Palmer (22 na 30) pamoja na Joao Pedro (43)

Cole Palmer anakuwa Mwingereza wa tatu kufunga goli katika Fainali ya FIFAClubWorldCup, wengine ni Wayne Rooney (2008) na Phil Foden (2023)

Chelsea inabeba kombe hilo kwa mara ya pili, ilitwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza Mwaka 2021 kwa kuifunga Palmeiras ya Brazil


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii