Rais mzee duniani atangaza kugombea tena urais Oktoba 12

Rais wa Cameroon Paul Biya (92), ambaye pia ni kiongozi mzee zaidi duniani, ametangaza kugombea urais kwenye uchaguzi wa Oktoba 12.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii, alihusisha uamuzi wake wa kugombea na simu nyingi za kusisitiza kutoka Mikoa kumi ya Nchi yake na kutoka ughaibuni.

Utawala wa karibu miaka 43 wa Paul Biya umekosolewa, huku wengi wakiutaja kugubikwa na ufisadi, ubadhirifu, utawala mbaya, na kushindwa kwa utawala wake kukabiliana na changamoto za usalama.

Ugombea wake katika uchaguzi huo unaofuatia talaka ya kisiasa ya hivi majuzi na washirika wakuu kutoka mikoa ya kaskazini, ambao walikuwa muhimu katika kusaidia kupata kura kutoka sehemu ya kimkakati ya nchi katika chaguzi zilizopita.

Ikiwa Bwana Biya atashinda urais atapata muhula mwingine wa miaka saba, itakuwa  mwaka umebakia Mwaka mmoja atimize umri wa karne moja (100) mwishoni mwa mamlaka hiyo.

Kabla ya tangazo lake, kulikuwa na wito unaoongezeka kutoka ndani na nje ya Cameroon kumtaka ajiuzulu kando na kutoa nafasi kwa sura mpya katika usukani wa taifa hilo la Afrika ya Kati.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii