Lissu kutoridhishwa na maombi ya upande wa Jamhuri kuahirisha kesi

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, ameonesha kutoridhishwa na maombi ya upande wa Jamhuri ya kuahirisha kesi yake ya uhaini, akisisitiza kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) tayari ameshalisoma jalada na kwa mujibu wa sheria lilipaswa kuwa mahakamani na ielezwe kuwa taarifa imeshapelekwa Mahakama Kuu na si vinginevyo.

Lissu ametoa kauli hiyo Julai 15 mwaka huu mahakamani wakati wa usikilizwaji wa Shauri Na. 8607/2025 linalomkabili akihoji sababu za kucheleweshwa kwa uamuzi wa DPP wa kuendelea au kuachana na mashitaka dhidi yake.

Lissu ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini amekuwa mahabusu kwa muda mrefu na ameeleza kuwa hali hiyo si jambo la kufurahisha kutokana na kudai kuwa yupo karibu na wafungwa wa kunyongwa hadi kufa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii