Kesi ya Lissu kusogezwa mbele hadi julai 30

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amerudishwa katika gereza la Ukonga, Dar es salaam baada ya kuahirishwa kwa kesi yake ya uhaini inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kesi hiyo imetajwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franko Kiswaga ambaye ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 30, 2025 kwa ajili ya kutajwa huku akiutaka Upande wa Serikali kuharikisha maombi yao waliyoyapeleka Mahakama Kuu kuhusu ulinzi kwa baadhi ya mashahidi wao.

Katika kesi hiyo Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini ambalo anadai amelitenda Aprili 3, 2025 kwa madai ya kuhamasisha kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii