Dkt,Samia kuongoza kikao cha Kamati Kuu julai 19

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitakachofanyika Julai 19 mwaka huu saa 4:00 asubuhi jijini Dodoma.

Kupitia taarifa iliyotolewa  Julai 15 mwaka huu  na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA. Amos Gabriel Makalla amesema Kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, inayoendelea kuketi jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa Sekreterieti hiyo inasalia Dodoma kwa ajili ya kupokea na kuchambua majina ya wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wa Jimbo na Viti Maalum, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya agenda za Kikao cha Kamati Kuu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii