Mrisho Mpoto msanii wa sanaa za maonesho na kughani, kupitia akaunti yake ya Instagram ametoa taarifa za kufiwa na mkewe ambaye alikuwa akiugua.
Akizungumza na mwandishi wa Jembe fmtz Mpoto amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa alikuwa akisumbuliwa na presha kwa muda mrefu.
Ameongeza kwamba Julai 15 mwaka huu alizidiwa ambapo alikimbizwa hospitali alikofikwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu.
Mpoto amesema kuwa msiba upo nyumbani kwake, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Julai 16, Yombo jijini Dar es Salaam.