Lissu leo kuendelea kusikiliza shauri lake mahakamani

Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, leo amepanda kizimbani katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, kuendelea na usikilizwaji wa shauri lake la maombi ya jinai alilofungua mahakamani hapo.

Lissu alifungua maombi ya kutaka mahakama hiyo kufanya marejeo juu ya maombi ya jamhuri kutaka kuficha mashahidi katika kesi ya uchochezi inayomkabili.

Lissu anakabiliwa na kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa YouTube, kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya mwaka 2015. 

Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini, ambapo shahidi mmoja tayari ametoa ushahidi.

Awali upande wa mashtaka uliwasilisha maombi ya baadhi ya mashahidi wake kutotambulika hadharani, jambo lililopingwa na mawakili wa Lissu wakidai sababu hazikutosha.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii