Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania, Mzee Steven Hizza, maarufu kwa wimbo wake wa “Tanzania Yetu Ndiyo Nchi ya Furaha,” amefariki dunia jioni ya jana Jumatatu katika eneo la Mwanzange, jijini Tanga.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na watu wa karibu na familia, zikieleza kuwa msanii huyo amefariki akiwa nyumbani kwake Mwanzange.
Aidha Mzee Hizza anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika muziki wa kizalendo, hususan kupitia wimbo wake uliopata umaarufu mkubwa na kuendelea kupendwa na vizazi mbalimbali nchini.
Hata hivyo taarifa zaidi kuhusu chanzo cha kifo chake na ratiba ya mazishi zinatarajiwa kutolewa na familia.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime