DCEA Yakamata Kilo 299.8 za Mirungi, Yateketeza Ekari 203 Same

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, imekamata kilogramu 299.8 za mirungi na kuteketeza ekari 203 za mashamba ya zao hilo katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Operesheni hiyo maalum iliyotekelezwa kati ya Februari 10 na 16, 2026 katika vijiji vya Marieni na Mhero, imefanikisha pia kukamatwa kwa watuhumiwa saba wanaodaiwa kujihusisha na kilimo na usambazaji wa dawa hizo za kulevya.

Akitoa taarifa, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema waliokamatwa ni pamoja na wale waliokaidi maagizo ya Serikali na kupuuza elimu iliyotolewa kuhusu athari za mirungi pamoja na fursa mbadala za kujipatia kipato halali.

Amesema mamlaka hiyo haitavumilia vitendo vya uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya, na itaendelea kushirikiana na viongozi wa ngazi zote kuanzia vijijini hadi mkoani ili kuhakikisha operesheni endelevu zinafanyika.

DCEA imeeleza kuwa juhudi hizo zinalenga kudhibiti kikamilifu tatizo la mirungi na kulinda afya na ustawi wa jamii mkoani Kilimanjaro.

Sasa ili kupata undani wa  taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa moja kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Geoge Kivumbi tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa. 

Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii