Mashambulizi ya Droni Kordofan Yazua Vifo 28 na Majeruhi Wengi

Mashambulizi katika soko kuu la kitongoji cha Sudri, Kordofan katikati mwa Sudan, yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 28 na kujeruhi makumi ya wengine, imesema Jumatatu jioni kundi la kutetea haki za binadamu, “Mawakili wa Dharura.”

Kundi hilo limeeleza kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka na kashifu shambulio hilo la droni dhidi ya raia, likisema kuwa hali inazidi kuwa mbaya katika Kordofan Kaskazini.

Hali hii inajiri huku vita kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF vikikaribia miaka mitatu, ambapo Umoja wa Mataifa unakadiria watu 40,000 kupoteza maisha na zaidi ya milioni 12 kuhamia kwenye kambi za wakimbizi.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii