Merz: Bado Hakuna Majibu ya Hatma ya Iran Baada ya Vita

Friedrich Merz amesema kuwa licha ya kukutana na Donald Trump mjini Washington, bado hajapata majibu ya wazi kuhusu hatma ya Iran baada ya kumalizika kwa vita.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Ujerumani, ZDF, mara baada ya mazungumzo yake na Trump, Merz amesema maswali mengi bado hayajajibiwa, ikiwemo mkakati wa Marekani wa baada ya vita nchini Iran.

Kabla ya hapo, Rais Trump alinukuliwa akisema kuwa “mmoja kati ya viongozi wa sasa” wa serikali ya Iran huenda akafaa kuchukua hatamu za uongozi, lakini hakufafanua ni kwa namna gani mchakato huo ungeweza kutekelezwa.

Kansela Merz alikuwa amezuru Marekani kwa mazungumzo kuhusu vita vya Ukraine na ushuru wa biashara kati ya mataifa hayo mawili, hata hivyo suala la vita vya Iran ndilo lililotawala majadiliano yao.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii