Wanamgambo wauwa wanajeshi 15 Benin

Kundi la wanamgambo wenye mahusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida limedai kuhusika na mauaji ya wanajeshi 15 kwenye kambi ya kijeshi kaskazini mwa Benin.

Wanamgambo hao wajiitao Kundi la Kuusaidia Uislamu na Waislamu (JNIM) limesema liliivamia kambi hiyo ya Kofouno karibu na mpaka wa Niger siku ya Jumatano.

Jeshi la Benin lilithibitisha vifo hivyo hapo jana. Msemaji wa jeshi, Kanali James Johnson, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mashambulizi hayo yamewajeruhi pia wanajeshi wengine watano.

Aidha Afrika ya Magharibi imekuwa ikikabiliwa na ongezeko la mashambulizi ya makundi yenye siasa kali, hasa nchini Burkina Faso, Mali na Niger, lakini katika miaka ya karibuni, mashambulizi hayo yameenea hadi Benin na Togo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii