Rubio kukutana na Netanyahu Februari 28

Afisa mmoja wa Marekani amesema kuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Marco Rubio atasafiri na kuelekea Israel wiki ijayo wakati ambapo mivutano inazidi kati yake na Iran.

Afisa huyo ambaye hakutaka kutajwa jina amesema Rubio ataelekea Israel Februari 28 kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Netanyahu ambaye alifanya ziara Washington wiki iliyopita kwa mazungumzo na Rais Donald Trump, kwa muda amekuwa akitaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya Iran na Juni mwaka jana aliamrisha kampeni kubwa ya kuishambulia Tehran kwa mabomu.

Aidha Trump aliishia kujiunga na kampeni hiyo ambapo aliamrisha kushambuliwa kwa vinu vya nyuklia vya Iran.

Ingawa siku ya Jumanne, Rais wa Marekani Donald Trump aliwatuma wajumbe wake kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Abbas Arraghchi huko Geneva, Uswisi.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii