Karibu watu 260,000 huuawa na ugonjwa wa uti wa mgongo kila mwaka duniani kote. Hii ni kulingana na utafiti uliochapishwa siku ya Jumamosi, Machi 28, katika Jarida la The Lancet Neurology. Maambukizi haya, ambayo huathiri ubongo, husababishwa na virusi au bakteria. Maendeleo yamepatikana, lakini bado hayatoshi. Malengo ya kimataifa hayatafikiwa kwa kiwango cha sasa.
Shirika la Afya Duniani limeweka lengo kubwa: kupunguza nusu ya visa vya ugonjwa wa uti wa mgongo na kupunguza vifo kutokana na ugonjwa huo kwa 70% ifikapo mwaka 2030. Hata hivyo, watafiti wanasema maendeleo ni yanapatikana hatua kwa hatua. Mnamo mwaka 2023, kulikuwa na visa zaidi ya milioni mbili na takriban vifo 260,000, theluthi moja wakiwa watoto.
Ingawa chanjo imesaidia kupunguza matukio ya ugonjwa huo tangu miaka ya 2000, ufikiaji wake hauna usawa sana. Katika baadhi ya nchi, 60% ya idadi ya watu wamechanjwa, ikilinganishwa na 30% katika nchi zingine.
Nchi maskini zaidi ndizo zilizoathiriwa zaidi Wanasayansi wanataja kile wanachokiita " (African Meningitis Belt) ni eneo maalum barani Afrika lenye kiwango cha juu zaidi cha maambukizi ya ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis) duniani," eneo linaloanzia Senegal hadi Ethiopia, kama lililo mstari wa mbele. Nigeria, Niger, na Chad zina viwango vya juu zaidi vya vifo. Nchi hizo ziko katika hatari kubwa zaidi kutokana na mifumo dhaifu ya huduma za afya.
Hali ya hewa pia ina jukumu muhimu. Wakati wa kiangazi, upepo wa Harmattan hubeba vumbi linalokera njia ya upumuaji na kuwezesha maambukizi. Uchafuzi wa hewa ndio sababu kuu ya hatari, lakini pia lakini pia kuzaliwa kabla ya wakati au kuzaliwa na uzito mdogo.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime