Nchini Niger, ni marufuku kusambaza picha za watu wanaopokea misaada, kama vile michango ya chakula. Shirika la taifa la Mawasiliano (ONC) linakumbusha vyombo vya habari na tovuti kuhusu sheria hii. Kulingana na ONC, hii ni muhimu ili kuhifadhi heshima ya watu husika. Wale wanaoshindwa kufuata sheria hii wanahatarisha athari za kisheria na kukabiliwa na adhabu.
Hakuna picha, hakuna video. Watu wanaopokea—kwa mfano—michango ya chakula nchini Niger, au aina nyingine yoyote ya misaada, hawapaswi kuonekana katika picha zinazosambazwa na vyombo vya habari, wala na mashirika au vyama vinavyopanga shughuli hizi. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Niger, awali, ilipiga marufuku kusambazwa kwa picha za wapokeaji wa chakula au misaada ya kijamii.
Wakati huu, ni Shirika la Kitaifa la Mawasiliano (ONC) linalorudia sheria hiyo katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa wiki iliyopita. Kwa mamlaka huko Niamey, picha hizi ni aibu kwa heshima na utu wa binadamu. idara kuu inayohusika na udhibiti, usimamizi, na uratibu wa shughuli za vyombo vya habari inakataza "picha zinazodhalilisha na kuaibisha ambazo zinachafua heshima ya watu binafsi."
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime