Marekani yaongeza tahadhari dhidi ya vitisho vya ujasusi

Wizara ya ulinzi ya Marekani, imeongeza kiwango cha tahadhari kuhusu vitisho vya ujasusi wa kigeni vinavyohusishwa na Israel . Haya ni kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zilizotolewa jana Jumamosi.

Shirika la Ujasusi la Ulinzi la Marekani (DIA) limesema uwezo wa Israel wa kufanya ujasusi wa kibinadamu na ukusanyaji wa taarifa za kijasusi kwa njia za kiufundi umefikia kiwango cha hatari kubwa. Haya ni kulingana na taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la NBC lililonukuu maafisa wa Marekani.

NBC pia imeripoti kuwa hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kuibuka kwa wasiwasi kwamba  Israel ilikuwa ikijaribu kuwachunguza kwa siri maafisa wa juu wa Marekani ili kupata taarifa kuhusu mijadala ya ndani na maamuzi ya utawala wa Donald Trump kuhusiana na migogoro ya Mashariki ya Kati.

Gazeti la The New York Times pia limeripoti madai ya juhudi za Israel za kusikiliza mawasiliano ya maafisa wakuu wa Marekani, akiwemo mjumbe mkuu wa mazungumzo wa Trump, Steve Witkoff, na afisa mkuu wa sera katika wizara ya ulinzi, Elbridge Colby.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii