Serikali ya Marekani inapanga kuangalia uwezekano wa kuelekeza mali za Iran kwenda mataifa ya Ghuba kwa ajili ya kugharamia ukarabati na fidia ya uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Iran.
Mataifa ya Ghuba ni nchi zilizopo katika eneo la Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf) Mashariki ya Kati Saudi Arabia, Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE), Qatar, Kuwait, Bahrain, Oman
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Iran kufanya mashambulizi dhidi ya Kuwait na Bahrain, huku Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, akitoa maagizo kwa timu maalum kufanya tathmini ya gharama za uharibifu uliosababishwa kwa washirika wa Marekani katika eneo la Ghuba.
Chanzo hicho kilisema Marekani pia inatafakari kutumia baadhi ya mali za Iran zilizozuiliwa au nyingine zinazohusishwa na taifa hilo kufidia gharama za.
Kauli hiyo imekuja baada ya mshauri wa kiongozi mkuu wa Iran, Mohsen Rezaei, kuiambia CNN kwamba makubaliano ya amani yanaweza kufikiwa iwapo Marekani itaachia dola bilioni 24 za mali za Iran zilizogandishwa.
Wakati huo huo, mazungumzo ya amani yanaonekana kusuasua licha ya Pakistan kutuma ujumbe maalum Tehran kwa ajili ya kuwasilisha barua kwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Mojtaba Khamenei.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime