Trump aitaka Ukraine kuacha kushambulia viwanda vya mafuta vya Urusi

Rais wa Marekani Donald Trump, Jumapili (Septemba 13) alitoa wito kwa mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kusitisha mashambulio dhidi ya miundombinu ya nishati ya mafuta ya Urusi.

Kwa mujibu wa Trump, mashambulio ya Kyiv yanaiathiri dunia pakubwa.

Ukraine imezidisha mashambulio dhidi ya miundombinu ya nishati ya Urusi katika siku za hivi karibuni na kusbabaisha kasi ya uzalishaji wa mafuta nchini humo kupungua na hata kushuhudiwa kwa uhaba wa gesi kote nchini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii