Oman yatangaza kuahirishwa kwa mazungumzo yaliopangwa kufanyika Jumatatu

Oman imetangaza kuahirishwa kwa mazungumzo yaliyopangwa kufanyika kuanzia siku ya Jumatatu, kati ya Iran na nchi za Ghuba, kujadili mzozo wa udhibiti wa mlango wa Bahari ya Hormuz, ambao umeendelea kuwa kitovu cha mzozo Mashariki ya Kati.

Oman inasema mazungumzo hayo, yaliyokuwa yamepangwa kufanyika katika mji wa Pwani wa Salalah, yataendelea siku nyingine na kuahirishwa huku, kunatoa fursa ya kuandaliwa kwa mazingira yatakayowezesha mazungumzo hayo kufanyika kwa utulivu.

Kuahirishwa huku kunakuja wakati Wizara ya Mambo ya nje ya Iran, ikisema mazungumzo ya Oman yaliombwa na nchi za Ghuba, na kukubaliwa na watawala wa Tehan na Muscat.

Mazungumzo hayo ambayo sasa haijafahamika, yatafanyika lini, yanalenga kujadili hatima ya mlango wa Bahari ya Hormuz, namna mzozo wa usimamizi kati ya Iran na Marekani unavyoathiri, usafirishaji wa gesi na mafuta na suluhu.

Mataifa yote ya ukanda wa Ghuba, ikiwemo Iraq yalikuwa yamepanga kuhudhuria mazungumzo hayo, ispokuwa Bahrain.

Iran na Marekani wamekuwa wakishambulia kuhusu eneo hilo la Bahari tangu kuanza kwa vita Februari tarehe 28. Iran inasisitiza kuwa Hormuz imefungwa huku Marekani ikisema, eneo hilo limefungiliwa na meli zinaweza kuendelea na safari zao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii