Netanyahu aukubali mpango wa amani wa rais Donald Trump

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema anaunga mkono pendekezo la mpango wa amani kwenye Ukanda wa Gaza baada ya mazungumzo na Rais Trump siku ya Jumatatu.

Hata hivyo wakuu hao wawili wametahadharisha kwamba Israel italazimika kuimaliza kazi iliyoianzisha kwenye eneo hilo ikiwa Hamas wataukataa mpango huo.

Bado haiko wazi ikiwa Hamas imeukubali ama itaukubali mpango huo ambao kulingana na taarifa yake bado haiujaupata. Hata hivyo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Trump alisema Marekani inaunga mkono kikamilifu hatua zitakazochukuliwa na Israel dhidi ya Hamas ikiwa wataupinga.

Ikulu ya White House jana Jumatatu ilitangaza mpango wa amani wenye pointi 20 ambazo ni pamoja na kuwanyang'anya kabisa silaha Hamas, Israel kujindoa taratibu kwenye Ukanda wa Gaza.

Kwenye mkutano na waandishi wa habaro Trump aidha alisema ataanzisha baraza la amani atakaloliongoza, litakalosimamia kipindi cha mpito kwenye Ukanda wa Gaza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii