Timu ya taifa ya Ivory Coast imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya AFCON 2025 baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3–0 dhidi ya Burkina Faso, ambayo sasa imeondolewa rasmi kwenye mashindano hayo.
Katika mchezo huo ulioshuhudia kiwango kikubwa cha ushindani mchezaji wa Manchester United Amad Diallo aliibuka kuwa shujaa wa mechi baada ya kufunga bao moja na kuongoza mashambulizi ya timu yake kwa ustadi mkubwa. Mabao mengine yalifungwa na Y. Didmande pamoja na B. Toure yaliyohakikisha Burkina Faso hawana nafasi ya kurejea mchezoni.
Kwa ushindi huo Ivory Coast sasa inajiandaa kuvaana na Misri katika hatua ya robo fainali mchezo uliopangwa kuchezwa Januari 10 mwaka huu huku mashabiki wakingoja kwa hamu pambano hilo lenye historia kubwa ya ushindani barani Afrika.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime