Tanzania yajiandaa kiuchumi ,na kimaandishi kwa AFCON 2027 inayo karibishwa pamoja na Kenya na uganda.

Tanzania pamoja na Kenya na Uganda,imepata nafasi ya kipekee yakuwa mmoja wa wenyeji wa mashindano ya kombe la mataifa ya kombe la mataifa ya Afrika ( AFCON) mwaka 2027,tukio kubwa la soka barani Afrika litakalo endeshwa kwa mara ya kwanza na nchi tatu kwa pamoja.

Hii ni fursa isiyowahi kutokea kwa nchi za Afrika mashariki na inatarajiwa kuwa na mfululizo wa manufaa ya kiuchumi na jamii kwa Tanzania.

Manufaa ya kiuchumi yanyotarajiwa:

1. Uenezaji wa utalii wa michezo na Tamaduni.

Tanzania inaendesha mikakati madhubuti ya kutumia AFCON 2027 kukuza utalii wa michezo pamoja na utalii wa tamaduni,wizara za serikali pamoja na wadau wa sekta ya utalii zinatarajia kwamba tukio hili litaleta maelfu ya watalii nchini,si tu kushuhudia mechi za soka bali pia kutembelea vivutio vya utalii kama serengeti,Mlima kilimanjaro na fukwe za bahari ,hii itapanua chanzo cha mapato kutoka maeneo mbalimbali ya utalii.

2:Kuongeza mapato kwa sekta ya huduma na biashara ndogo.:

Kuonggezeka kwa wageni tutazidisha mahitaji ya malazi ,mikahawa,usafiri,na huduma nyingine za kibiashara .

Hii ina maana kwamba biashara ndogondogo kupitia usafiri,wauzaji wa bidhaa na vyakula ,pamoja na huduma nyingine zinazohusiana na watalii na mashabiki wa soka.

3: Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu:

Serikali tayari imeanza au iko katika maandalizi ya ujenzi wa miundombinu muhimu kama ujenzi wa viwanja vipya vya michezo . 

Miji kama Arusha na Dodoma zinatarajiwa kupata uwanja mpya wa kisasa utakaotumika katika mashindano hayo,na hivyo kuchochea uwekezaji wamabilioni ya fedha na kujenga ajira kwa wahandisi,mafundi,na wafanyabiashara wandani.

4. Kuibua fursa za uwekezaji wa kigeni kwakuwa AFCON ni tukio lenye hadhira kubwa barani Afrika na dunia,Tanzania itapata mwangaza wa kimataifa unaoweza katika wawekezaji wa kigeni kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo hoteli,mikahawa,na miradi ya burudani.

Kwaupande mwingine ,kufanya biashara ya kimataifa kutazidi kukua kutokana na uwekezaji wa nje.

Changamoto na mikakati ya kukabiliana na zao:

Hata hivyo,maandalizi ya kufanikisha AFCON 2027 hayako bila changamoto . 

Tanzania pamoja na washirika wa kupanga uzingatie ukamilifu wa miundo mbinu ,vyanzo vya fedha za kutosha ,na uhamasishaji wa wadau wote ili kuhakikisha manufaa ya kiuchumi yanadumu hata baada ya mashindano.

Serikali imetakiwa pia kuhakikisha usalama,huduma bora na ustawi wawageni ili kutengeneza taswira nzuri ya nchi kwa wageni na wawekezaji.

Tayari kwa Baadaye Endelevu:

Wadau wa utalii na aekta ya huduma wanahoji kwamba tukio hili linapaswa kutumika si kwa mashindano tu,bali kama msingi wa kuendeleza utalii wa michezo ,utalii na tamaduni ,na shughuli za kiuchumi kwa miaka ijayo. 

Pamoja na changamoto ,matarajio ni makubwa kwamba AFCON 2027 itakuwa ni mlango wa mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa Tanzania.

Kwa yote haya,Tanzania inakazia macho juu ya AFCON 2027 Kama fursa ya kugusia uchumi kupitia sekta mbalimbali na kuchangia ukuaji endelevu wa Taifa.

Na: Mbeki Mbeki 

Kagera.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii